DI MARIA AFURAIA UHAMISHO WA KUJIUNGA NA PSG





Angel Di Maria asema kuwa anafuraha kujiunga na klabu ya Paris St-Germain kutoka Manchester United ikiwa ni mwaka mmoja baada ya mashetani wekundu kumnunua kwa uhamisho ulioweka rekodi katika ligi ya Uingereza kwa Euro milioni 59.7 kutoka Real Madrid.

Nyota huyu mwenye umri wa miaka 27 alifanyiwa vipimo vya afya huko Qatar na kukamilisha uhamisho wake uliogharimu kiasi cha pauni milioni 44.3.
Baada ya uhamisho huo kukamilika Di Maria alisema ana furaha kujiunga na Paris St –German .
Lakini vilabu vya Manchester United na PSG havijatangaza rasmi kukamilika kwa uhamisho huo .


Di Maria alijiunga na mashetani wekundu msimu uliopita akitokea Real Madrid ambapo alicheza michezo 32 na kufunga mabao 4.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment