Gwiji wa soka kutoka nchini Brazil Edson Arantes do Nascimento  maarufu kama Pele ameruhusiwa kutoka hospitali kufuatia kufanyiwa upasuaji wa tezi dume na madaktari wamesema ni baada ya afya yake kuimarika.

Albert Einstein ni hospitali iliyopo jijini Sao Paulo ambapo mchezaji huyo nguli mwenye umri wa miaka sabini na nne alikuwa aki patiwa matibabu.Hospitali hiyo imetoa picha ya Pele akitabasamu huku amevaa mavazi ya kimichezo na akipunga mkono hakuwa peke yake bali ameambatana na mpenzi wake Marcia Cibele Aoki.
Pele ni Mchezaji pekee aliye shinda mataji matatu ya kombe la dunia na alifanyiwa taratibu za upasuaji huo siku nne zilizopita ili kuongeza ukubwa wa kibofu cha mkojo.Matokeo ya vipimo vilivyo chukuliwa yameonyesha kuwa hakuna uvimbe wa aina yoyote kwani ugonjwa ulikuwa katika hatua za awali.Nguli huyo ambaye ni alama ya kimataifa ya michezo amesumbuliwa na maradhi mengi katika miezi michache ya hivi karibuni.
Kwani aliwahi kufanyiwa upasuaji kwenye figo ili kuondoa mawe mnamo mwezi Novemba, na pia alikutwa na maambukizi ambayo yalimlazimu kulazwa katika hospitali yenye kitengo cha huduma ya uangalizi wa hali ya juu kwa siku kadhaa.

Pele alitajwa kama mwanamichezo bora wa karne baada ya mkutano wa kimataifa wa Olimpiki mnamo mwaka 1999.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment