Katika ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga Borussia Dortmund waliwakaribisha wapinzani wao Bayern Munich katika dimba la Siguna Iduna Park


Mchezo huo uliomalizika muda mfupi uliopita umeshuhudia Bayern wakipata ushindi mgumu wa goli 1-0 dhidi ya vijana wa Jurgen Klopp.
Robert Lewandoski mchezaji wa zamani wa Dortmund ndio aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa timu yake ya zamani baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira uliokolewa na kipa wa Dortmund mapema katika kipindi cha kwanza.

Kwa matokeo hayo Bayern Munich wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani.

Matokeo mengine ya Bundesliga.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment