OSCAR PISTORIUS APANDISHWA HADHI GEREZANI

Oscar pistorius akiwa amekumbatiana na shangazi yake.

Kuhusiana na mwanariadha Oscar Pistorius aliyeko kifungoni, imeelezwa kwamba sasa anaweza ama kuruhusiwa kukumbatiana na wageni wake na hata kuwabusu wanaomtembelea ,anaruhusiwa kusikiliza redio na hata kuvaa vitu vya thamani ikiwemo vito vya thamani akiwa ndani ya gereza,,

Mtuhumiwa huyo wa mauaji,amepewa ruhusa nyingine ya kuwa huru kupiga simu atakavyo,vile vile bajeti yake inayodaiwa kuwa kubwa, imekubaliwa aweze kununua vyoo atakavyo na hata akitaka chipsi ataletewa,na huu ni uamuzi wa bwana jela anaye angalia wafungwa na hadhi zao naye Pistorius yuko kundi B.
Ikumbukwe kwamba Oscar alimuua mpenzi wake mnamo mwezi kama huu na siku inayotajwa kuwa muhimu ulimwenguni tarehe ya kumi na nne Valentine's Day,mwaka jana akiwa nyumbani kwake.
Akiwa jela Pistorius anajaribu kuyazoea mazingira ya jela na inamuwia vigumu kukubali kuwa ameupoteza uhuru wake, na pia kuonekana kama tishio la usalama na hivyo yumo ndani.
Msemaji wa familia ya Pistorius mwanamama,Annalise Burgess, amemzungumzia mwanariadha huyo aliyekuwa maarufu duniani kiasi cha kupachikwa jina la Blade Runner,sasa amepandishwa hadhi na kuwa daraja la A .
Familia ya Oscar ina Whatsapp group la familia yao ambalo linafuatilia taarifa zote za mwanariadha huyo na pia hutumia akaunti hiyo kujadiliana masuala ya biashara za familia.
Inaelezwa kuwa watu wanaoongoza kumtembelea Oscar Pistorius Jela ni kaka na dadake Aimee Carl na wakiisha kuonana naye hutuma taarifa na picha katika kundi hilo na kinachoendelea kumhusu yeye gerezani.
Kupandishwa kwa Oscar kuna maanisha kuwa anaruhusiwa kutembelewa na wageni zaidi ikiwemo familia yake.Hapo mwanzo kila anayemtembelea huzungumza naye kwa njia ya simu akiwa ametengwa na mgeni wake na vioo, na hakuruhusiwi kuguswa,lakini mambo sasa yamebadilika.
Sasa Oscar mwenye umri wa miaka ishirini na nane, anaweza kuwakumbatia jamaa zake wamtembeleapo,na muda wa kumuona umeongezwa kutoka saa mbili hadi tatu kwa mwezi,na wageni wamtembeleao bado wanakabiliwa na sheria ya kupekuliwa kabla ya kuonana na mfungwa huyo ambaye bado anatakiwa kuvaa sare za jela zenye rangi ya samawati ama ita orange.
 
Suala la hadhi ya Oscar kupandishwa daraja limewakera wafungwa wenziwe walioko kwenye gereza la Death Island: lililotengwa,ambalo limezungukwa na nyaya za umeme wamelalama kuwa mwanariadha huyo mlemavu anapewa hadhi ya kifalme kwa muda mfupi sana ilhali wao wanataabika muda mrefu gerezani.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment