Wanafamilia ambao wamekumbwa na mauti kwa pamoja.

Maafisa wa polisi mjini Carolina kazkazini nchini Marekani wamemkamata mtu mmoja baada ya wanafunzi watatu waislamu kupatikana wamefariki nyumbani mwao..

Miili ya Deah Barakat,mkewe Yusor Mohammed Abu salha na dada yake Razan Mohammed Abu salha ilipatikana siku ya jumanne ikiwa na majeraha ya risasi katika vichwa .
Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 46 tayari amefunguliwa mashtaka kutokana na mauaji hayo.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kubaini iwapo mauaji hayo yanatokana na chuki.
Swala kwamba wanafunzi waliouawa ni waislamu limezua uvumi katika mitandao ya kijamii iwapo mauaji hayo ni ya kidini au la.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kwamba uhalifu huo ulitekelezwa kutokana na mzozo unaondelea kuhusu uegeshaji wa magari,maafisa wa polisi wa Chapell wamesema.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment