Kamati Kuu ya CCM (CC) inakutana Jumamosi wiki hii huku mambo muhimu sita yakitarajiwa kujadiliwa, likiwamo suala la makada wa chama hicho waliopewa adhabu ya onyo kali kwa kuanza kampeni za urais mapema na ukiukaji wa maadili,,

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, licha ya kutoeleza ajenda za kikao hicho, ilisema kitafanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete kuanzia saa 4 asubuhi.
Kikao hicho kinafanyika wakati upepo wa kisiasa ndani ya chama hicho ukiwa haujatulia huku kukiwapo masuala mazito ya kitaifa yanayotikisa medani za kisiasa, likiwamo suala la uandikishaji wapiga kura, maandalizi ya kura ya maoni za kupitisha Katiba Inayopendekezwa na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, ambayo yameelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa hayawezi kukwepeka katika kikao hicho.
Adhabu kwa wagombea
Itakumbukwa kuwa kikao hicho kitafanyika ikiwa ni siku 10 baada ya kukamilika tarehe ya mwisho ya adhabu kwa makada sita wa CCM, waliokuwa wakitumikia adhabu ya miezi 12 kwa ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais.
Kikao kilichopita cha CC kilibainisha kuwa baada ya muda wa adhabu zao kuisha, Kamati Kuu ingefanya tathimini kuona iwapo wagombea hao walizingatia masharti ya adhabu zao na endapo kungekuwa na ambao hawakuzingatia masharti adhabu zao zingeongezwa.
Nnauye alithibitisha kuwa muda wa adhabu hiyo ulikuwa ukingoni na kuwa viongozi hao wangefanyiwa tathmini na kamati ndogo ya maadili ili kubaini iwapo adhabu hiyo ilitekelezwa ipasavyo.
Makada waliokuwa wakitumikia adhabu hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Waziri wa Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
 
Kikao hicho huenda pia kikazungumzia mwenendo wa uandikishaji wa wapiga kura katika Daftari la Kudumu kwa kutumia teknolojia ya alama za vidole (BVR), iliyozinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
CCM, ni miongoni mwa vyama vya siasa nchini vinavyoungana na vyama vinavyounda Umoja ya Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuhoji mara kwa mara ufanisi wa mfumo wa BVR katika kuandikisha wapigakura kutokana na historia yake isiyoridhisha.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment