ALI KIBA AFUNGUKA KUHUSU KUTOELEWANA NA DIAMOND

Ali kiba

Hatimaye staa wa Bongofleva Ali Kiba amekiri kuwa yuko katika bifu na mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz kwa zaidi ya miaka mitatu sasa..
Kauli hiyo ya Ali Kiba inapingana na ile ya hivi karibuni iliyowahi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati za bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisisitiza kuwa wanamuziki hao hawana tofauti zozote na kwamba ni watu tu ndio wanakuza suala hilo.
Hata hivyo, juzi Ali Kiba alikubali kuwa ni kweli kuna ugomvi baina yao, huku akisisitiza kwamba tofauti yao ilianza mwaka 2012. Wakati Ali Kiba akifunguka kuhusu bifu hilo hali imekuwa tofauti kwa Diamond ambapo amekaririwa mara kadhaa kuwa hana tofauti yeyote na mwanamuziki huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganisha Kundi la Kigoma All Stars.
Swali: Nini chanzo cha bifu lako na Diamond?
Ali Kiba: Hakuna kiini kwa sababu nadhani hayo mimi aaah.…Kiukweli haya tuliyamalizaga muda mrefu …Labda watu wahisi kwamba kipindi kile alichonifuta katika wimbo wake (alisema bila kufafanua jina la wimbo) na yeye alivyosema kwamba nimemfuta katika wimbo wangu ‘Single Boy’, mimi sijawahi kurekodi na Diamond katika wimbo wangu hata mmoja na huo niliimba na Lady Jaydee.
Yeye ndiye aliyesema kwamba nilimfuta katika wimbo ule, ila ukweli ni kwamba hatukuwahi kuingia pamoja studio, nilimshauri tufanye wimbo mwingine lakini siyo ule kwa sababu nimeshaimba na Lady Jay Dee.





Credit; Mwananchi
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment