John Mnyika ambaye ni mbunge wa jimbo la Ubungo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara akihutubia katika mkutano wa hadhara. |
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika amesema mchanganyiko wa viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika ngazi ya Serikali za Mitaa ni dalili tosha ya kuking’oa madarakani Chama cha Mapinduzi.
Mnyika alisema hayo katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Mabibo, Dar es Salaam uliokuwa na lengo la kuwashukuru
wakazi wa kata hiyo kuwachagua viongozi wa Ukawa.
Lakini pia aliongeza kuwa CCM isitarajie mteremko katika Uchaguzi
Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwa kuwa Ukawa wana kila
sababu ya kuibuka washindi.
“Waswahili wanasema dalili njema huonekana asubuhi
na umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, hivyo CCM ijiandae kuachia
madaraka kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge na urais.
“Huu mseto wenzetu unawapa shida kweli kweli na
hautovunjika hadi tunahakikisha tunaingia Ikulu Oktoba mwaka huu,”
alisema Mnyika, huku akishangilia na wananchi hao.
Mnyika ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
Bara, aliwataka wenyeviti hao kufanya kazi kwa uadilifu, ikiwamo
kuitisha mikutano ya mara kwa mara na wananchi ili kusikiliza kero zao
na kuzitatua kwa wakati.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabibo, Francis Mayunga
alikuwa mwenyeji wa mkutano huo, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano
kwa safu hiyo mpya ya uongozi wa mtaa huo ili waletewe maendeleo
waliyoyakusudia.
Credit; Mwananchi
Credit; Mwananchi
0 comments :
Post a Comment