Mwanariadha wa kimataifa kutoka Jamaica Usain Bolt. |
Wanasayansi wanasema kwamba wanaweza
kueleza kasi ya mwanariadha maarufu sana duniani Usain Bolt inatokana
na nini kwa kutumia hisabati au hesabu.
Bolt alivunja rekodi kwa kumaliza mbio za mita 100 kwa sekunde 9.58 wakati wa mashindano ya kimataifa mwaka 2009 mjini Berlin. Na hio ndio rekodi ya dunia.
Wanasayansi hao wanasema utafiti wao unafafanua kwamba nguvu na uwezo wa kimwili wa Bolt kustahimili upepo inatokana na urefu wake wa futi 6 inchi 5.
Hata hivyo wanasayansi hao wanasema bado wanafanya uchunguzi kujua kinachowafanya wanariadha wazuri kama Bolt kukimbia kwa kasi.
Kulingana na utafiti wa wanasayansi hao waliotumia hesabu,kasi ya Bolt ya sekunde 9.58 mjini Berlin iliwezekana baada ya mwanariadha huyo kukimbia mita 12.2 kwa sekunde sawa na kasi ya mita 27 kwa saa.
Walisema kuwa mwili wa Bolt ulipata kasi yake pindi alipoanza kukimbia chini ya sekunde moja na hiyo ilikuwa nusu tu ya kasi yake yote.
Wanafizikia hao wanasema hii ina maanisha kuwa hapo ndipo hewa hupunguza nguvu zake za kusongesha vitu.
Pia waligundua kwamba chini ya asilimia nane ya nguvu za misuli yake ilitumika wakati alipoanza kukimbia.
Usain Bolt akishangilia kwa mtindo wake baada ya kushinda. |
''Ni vigumu sana kuvunja rekodi siku hizi, hata kwa sekunde moja kwani wanariadha wanahitajika kutumia nguvu nyingi sana dhidi ya upepo ambao huongezeka kwa kila ongezeko la kasi, '' walisema wanafizikia waliofanya utafiti huo.
John Barrow wa chuo kikuu cha Cambridge alisema kwamba kasi ya Bolt pia ilitokana na urefu wa hatua zake za miguu licha ya kuanza mbio kwa kuchelewa kila wakati kipenga kilipopigwa.
"misuli yake inamsaidia sana kuongeza kasi licha ya kwamba mwenyewe ana kasi.''
Wanasema kwamba Bolt ana uwezo mkubwa wa kuvunja rekodi zaidi ikiwa ataanza mbio zake bila ya kuchelewa.
Credit; BBC
0 comments :
Post a Comment