RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Jakaya Mrisho Kikwete Raisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Rais Jakaya kikwete wa Tanzania ametangaza mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.
Rais amewateua mawaziri wanane wapya pamoja na manaibu watano..

Tangazo hilo lilifanywa na katibu katika ikulu ya rais balozi Ombeni Sefue.
Mabadiliko hayo yanajumuisha wadhfa wa waziri wa nishati na madini Profesa Muhongo ambaye amejiuzulu mapema pamoja na wadhfa wa waziri wa ardhi ambao uliachwa wazi baada ya kupigwa kalamu kwa Anna Tibaijuka.
Mawaziri hao wawili wanahusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo ilimshinikiza mwanasheria mkuu pia kujiuzulu.Nafasi ya Profesa Muhongo imechukuliwa na aliyekuwa naibu wa waziri wa ardhi, George Simbachawene.
Rais Kikwete amewaapisha mawaziri hao wapya katika tangazo lililorushwa hewani na runinga ya taifa moja kwa moja.
Hii ndio orodha ya mawaziri walioteuliwa
MAWAZIRI
George Simachawene waziri wa nishati na madini
Mary Nagu- waziri wa nchi [ofisi ya rais] mahusiano na uratibu
Christopher chiza -waziri uwezeshaji na uwekezaji
Harisson Mwakyembe[waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki]
William Lukuvi -waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Steven Wasira -waziri wa kilimo chakula na ushirika
Samwel Sita -waziri wa uchukuzi
Jenista Muhagama -waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera uratibu na bunge
MANAIBU WAZIRI
Stephen Masele -naibu waziri ofisi ya makamu wa rais muungano
Angela Kariuki -naibu waziri wa ardhi nyumba na makaazi
Ummi Mwalimu- naibu waziri wa katiba na sheria
Anna Kilango - naibu waziri wa elimu na mafunzo ya kiufundi
Charles Mwijage-naibu waziri wa nishati na madini.



Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment