MTOTO WA RAILA ODINGA AFARIKI

Fidel Odinga mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga enzi ya uhai wake



Fidel Odinga mwana wa aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga amepatikana akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen.

Maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha mfanyabiashara huyo ambaye pia amekuwa akionekana katika ulingo wa kisiasa.
Maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonyesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa jumamosi na alirudi mapema jumapili.
Haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake.
Kundi la wabunge pamoja na maseneta liliwasili katika nyumba ya Raila baada ya kupata habari hizo.
Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment