MKIA WA NDEGE WAPATIKANA BAHARINI

Mabaki ya mkia wa ndege ya Air Asia yakiwa ndani ya bahari ya Java.


Mkia wa ndege ya Air Asia iliyoanguka umepatikana kwenye bahari ya Java, kikosi kilichokuwa kikisaka ndege hiyo kimeeleza.

Mkia huo wa ndege hutunza visanduku vyeusi vinavyorekodi mawasiliano ndani ya ndege ambavyo vingeweza kuwasaidia wachunguzi kubaini chanzo cha ajali.
Sehemu hiyo ya mabaki ya ndege ilionekana kwenye eneo la ziada lililoongezwa kwenye operesheni ya kutafuta ndege hiyo.
Air Asia ilipotea ilipokuwa ikitoka Surabaya, Indonesia kwenda Singapore tarehe 28 mwezi Desemba ikiwa na Watu 162.
Hakuna manusura yeyote aliyepatikana.
Mpaka sasa miili 40 pekee imepatikana lakini Mamlaka zinaamini kuwa abiria wengi zaidi wamenasa ndani ya ndege hiyo.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment