Ronaldo akiwa ameweka pozi na mtoto wake katika sanamu hiyo.
Hapa akiwa na familia yake na watu kutoka kisiwani Madeira.


Cristiano Ronaldo amezindua sanamu yake ya kumuenzi kwa mafanikio yake, katika mji aliozaliwa wa Funchal kwenye Kisiwa cha Madeira.

Akizungumza katika uzinduzi huo maalumu huku akizungukwa na Familia yake pamoja na Maelfu ya Mashabiki, Ronaldo alieleza “Huu ni wakati maalumu kwangu, kuweka Sanamu yangu!”
Dolores Aveiro mama yake Ronaldo aliongeza kwa kusema"Ronaldo hajawahi kusahau asili yake”
Sanamu hiyo yenye Urefu wa Mita 3.4 ni sehemu ya mkusanyiko wa Mataji na Tuzo mbalimbali ambazo amezitwaa katika maisha yake ya Soka na kuhifadhiwa kwenye Makumbusho yake maalum hapo Kisiwani Madeira zikiwemo tuzo za Ballon d'Or.
Ronaldo huu umekua ni msimu mzuri sana kwake na amefunga jumla ya magoli 34 katika michezo 27 msimu huu, na ni mmoja kati ya wachezaji waliochaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia katika mwaka huu, huku akiwa mchezaji anayetazamwa kwa umakini zaidi kwenye tuzo hizo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment