11 WAPOTEZA MAISHA KWA KUKANYAGANA

Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufanyika katika uwanja wa soka.

Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga baadhi ya milango ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea vifo hivyo alihuzunika sana.




Credit; BBC
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment