
Cristiano Ronaldo amezidi kuudhihirishia ulimwengu kwamba mbali ya kuwa bora kwenye soka, bado ana rekodi nyingine kubwa ambazo zinafanya jina lake kuwa kwenye rekodi mbalimbali ambazo zitadumu milele duniani
Takwimu za mtandao wa goal.com. zinaonyesha
staa huyo kuwa NUMBER 1 kwenye orodha ya mastaa wa soka wanaoongoza kwa
kuingiza pesa nyingi zaidi duniani na kuwa na utajiri mkubwa.
Takwimu za mtandao huo zinaonyesha Ronaldo ana utajiri wa paundi milioni 210 akimuacha nyuma mpinzani wake anayeshikilia nafasi ya pili Lionel Messi mwenye utajiri wa paundi 200.
Utajiri wa Ronaldo haupatikani kwa soka lake uwanjani pekee, ana madili mengine mengi ikiwemo kuwa balozi wa kampuni mbalimbali kama Toyota, Nike na Herbalife ambazo zimeweka pesa kwa staa huyu ili awe Balozi wao rasmi kutangaza bidhaa zao.
Na hapa ni orodha yote ya wachezaji wenye pesa nyingi.
1. Cristiano Ronaldo
Mchezaji wa Real Madrid: Huyu ndiye mchezaji bora wa dunia na ameendelea kushikilia rekodi yake ya nafasi ya kwanza, ana utajiri wa Euro milioni 210
2. Lionel Messi

Ni mchezaji wa Barcelona: ana utajiri wa Euro milioni 200
3. Neymar Da Silva Santos Jr

Staa wa soka toka Brazil ambaye anachezea klabu ya Barcelona: Utajiri wa Euro milioni 135
4. Zlatan Ibrahimovic

Striker wa Klabu ya Paris Saint- German Fc: Ana utajiri wa Euro milioni 105
5. Wayne Rooney

Mshambuliaji wa muda mrefu Klabu ya Manchester United: Utajiri wake ni Euro milioni 103
6. Ricardo Kaka

Ni kiungo wa timu ya Taifa ya Brazil na Orlando City: Ana utajiri wa Euro milioni 96
7. Samuel Eto’o

Jamaa anachezea Klabu ya U.C Sampdoria: Utajiri wake ni Euro milioni 87
8. Raul Gonzalez

Mshambuliaji wa timu ya Al Sadd SC: Ana utajiri wa Euro 85
9. Ronaldinho (Gaucho)

Ni kiungo wa Queretaro F.C: Ana utajiri wa Euro milioni 83
10. Frank Lampard

Ni kiungo wa Manchester City: Ana utajiri wa Euro milioni 80
0 comments :
Post a Comment