Kulingana na mtandao wa Goal.com Lucas Podolski anasema kuwa mkufunzi wa klabu hiyo Arsene Wenger anampuuza.
Mshambuliaji huyo amechezeshwa mechi nne pekee katika ligi ya Uingereza msimu huu,huku akianzishwa katika mechi ya kombe la Carling ambapo Arsenal ilipoteza kwa Southampton mnamo mwezi Septemba.
Lucas Podolski aliacha kuchezeshwa mara kwa mara katika klabu yake.
Mchezaji huyo aliyetoka klabu ya Koln nchini Ujerumani alisema kwamba anapanga kufanya mazungumzo na Arsenal kuhusu hatma yake mwezi january na akasisitiza tena siku ya ijumaa wakati taifa lake liliposhinda.
''Nimekuwa nikiichezea Arsenal kwa dakika chache ,niko tayari kuionyesha Arsenal kile naweza kuifanyia ,lakini fursa hiyo haipatikani'',alisema Podolski.
Podolski amecheza dakika 90 wakati Ujerumani ilipoicharaza Gibraltar mabao 4-0 katika mechi za kuwania kufuzu katika dimba la Ulaya,lakini mkufunzi Joachim Low anataka mchezaji huyo kuanza kucheza mechi nyingi kwenye klabu yake.
-
Blogger Comment
-
Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments :
Post a Comment